SIRI ILIYOPO KWENYE UKIMYA WA WATU WAKIMYA NA WAPOLE INTROVERT
Silence is not weakness, it’s preparation.
Watu wengi wanaamini kwamba nguvu inaonekana kwenye kelele na kuongea sana kama mtu mwenye mamlaka.
Mtu anayesema sana, anayejionyesha sana, anayependa kila mtu ajue hatua zake mara nyingi ndiye anayeonekana kama mwenye kujiamini.
Lakini kuna aina nyingine ya nguvu ambayo haipigi kelele.
Na hiyo ni nguvu ya mtu anayekaa kimya.
Ukimya ambao watu wengi wanauona kama ni udhaifu kumbe ndani yake kuna mchakato mkubwa ambao unaendelea.
Kwa sababu wakati mwingine mtu akiwa kimya sio kwamba hana cha kusema…
Ni kwamba anachagua muda sahihi wa kusema.
Sio kila vita vinashindwa kwa kupiga kelele. Kuna vita vinashindwa kwa akili, subira, na uwezo wa kusubiri wakati sahihi wa kuongea.
Sisi watu wakimya (introvert) hua tunautumia ukimya wetu na kwenye muda wetu mwingi wa upweke ku…
1. Kusoma mchezo.
Sisi ni watazamaji zaidi kuliko washiriki.
Tunaangalia namna watu wanavyoongea, wanavyotenda, wanavyobadilika kulingana na mazingira.
Tunajifunza kwamba sio kila tabasamu lina maana ya urafiki, na sio kila ukimya wa mtu una maana ya udhaifu.
Wakati wengine wanaongea sana, sisi tunakusanya taarifa.
Tunaangalia vitu vidogo ambavyo watu wengi hawavioni.
Macho, sauti, mwendo, tabia.
Kwa sababu mtu anayesikiliza zaidi mara nyingi hujua zaidi. Yani sisi hua Hatuaji dogo wala kubwa, kila data ina sehemu yake kwenye kichwa chetu.
2. Kupanga hatua zetu.
Watu wengi hupenda kuonyesha mbegu kabla haijawa mti.
Lakini watu wakimya mara nyingi hujifunza kitu kimoja:
Kuna vitu vinakua vizuri zaidi vikikaa siri.
Mipango yetu hatuipeleki kila mahali.
Ndoto zetu hatuzitangazi kwa kila mtu.
Tunajua kwamba sio kila mtu anayesikia maono yako atakutakia kuona yakitimia.
Kwa hiyo tunafanya kazi kimya kimya.
Tunajenga.
Tunajifunza.
Tunajirekebisha.
Halafu siku ikifika, matokeo yanaongea kwa niaba yetu. Okopa sana hapa, tunaweza kucheka na wewe huku tukikupangia mpango wa kulipiza kisasi kosa ulilotufanyia miaka kumi iliyopita, hahaha… sio kweli.
3. Kujijenga ndani.
Upweke wetu sio lazima uwe huzuni.
Mara nyingine ni sehemu ambayo tunajikusanya tena.
Ni muda wa kujiuliza:
Nataka kuwa nani?
Ninaenda wapi?
Nini kinanizuia?
Kwa nini niko hapa?
Ni vitu gani vinanifanya nirudie makosa yale yale?
Kwenye ukimya ndipo mtu anaanza kujifahamu.
Kwa sababu dunia ikiwa na kelele nyingi, ni vigumu kusikia sauti yako mwenyewe.
Wengi hua wanakosea na kutuita overthinker ila ukweli ni kwamba mara nyingi hua tuko tunayafikiria mambo yote yanayoendelea kwenye maisha yetu.
4. Kuchaji akili na roho.
Kila siku tunakutana na nguvu tofauti za watu, matatizo, presha, watu wenye negative mindset na mazingira tofauti tofauti…
Na kwa mtu anayependa utulivu, muda wa kuwa peke yake ni kama kurudisha mfumo kwenye mstari.
Ni kama simu yenye betri ndogo ukiipeleka kwenye charger.
Sio kwamba simu imeharibika.
Inahitaji tu nguvu mpya ili iweze kufanya kazi vizuri.
Ndio maana watu wakimya wakirudi, mara nyingi wanarudi wakiwa na focus kubwa zaidi.
Comeback zetu hua ni za moto sana.
5. Kujiponya bila makelele.
Sio kila maumivu yanahitaji mashahidi.
Kuna vitu mtu anavipitia kimya kimya na vinamfundisha zaidi kuliko maneno ya watu mia.
Ukimya unampa mtu nafasi ya kukutana na nafsi yake mwenyewe.
Kukubali makosa yake.
Kujifunza.
Kukomaa.
Na kutoka akiwa mtu tofauti.
Lakini kumbuka…
Kuwa kimya haimaanishi huna nguvu.
Simba hakimbii huku akitangaza kwamba yeye ni simba.
Anatembea taratibu kwa sababu anajua nguvu yake.
Kuna watu wanaonekana kimya leo, lakini ndani yao kuna mtu anayejengwa kwa ajili ya kesho.
Kwa sababu wakati mwingine…
Ukimya sio mwisho wa mchezo.
Ukimya ni maandalizi kabla ya hatua kubwa.
Najua kuna mambo mengi ambayo yanaendelea kichwani mwako, changamoto za hapa na pale but trust me dakika 30 tu za kila siku kukaa kwenye ukimya huku uki-analyze mawazo yako na kila kitu kinachoendelea kwenye maisha yako kunaweza kutatua nusu ya matatizo yako. Kwenye ukimya unaweza…