Je, ni kweli kuwa G-55 inapinga msimamo wa Chadema?
Hapana. G-55 haipingi msimamo wa Chama, bali imekuja na ushauri bora wa kutekeleza msimamo wa No Reforms, No Election wa Chama.
Kwanza, G-55 inaunga mkono madai ya reforms. Pili, inakisihi Chama kishiriki uchaguzi si kwa nia ya kupinga mpango wa kuzuia uchaguzi, bali kwa kutaka mpango huo ufanyike tu pale penye hujuma na utekelezwe kwa ufanisi zaidi.
Kimkaķati, G-55 inaamini ni rahisi kuzuia uchaguzi (No Election) tukiwa ndani ya uchaguzi, kuliko nje ya uchaguzi, maana mtandao mpana wa wagombea wetu, mawakala wetu na timu zetu za kampeni utasaidia sana kuzuia uchaguzi kwenye maeneo mahsusi yanayoelekea kufanyiwa hujuma. Kwa mantiki hiyo, G-55 inaunga mkono No Reforms, No Election lakini imeshauri mkakati na mbinu tofauti ya utekelezaji (advanced approach)
Kwanini G-55 imeshauri hivyo?
Kushiriki uchaguzi kuna faida nyingi, kubwa kuliko yote ni kuepusha CCM kupita bila kupingwa na angalau kuhakikisha tunashinda au tunapata matokeo yatakayosaidia kulinda uhai na ustawi endelevu wa Chadema yetu, huku mapambano zaidi ya kidemokrasia yakiendelea. Chama kilicho nje ya uchaguzi hakiwezi kukua. Change is a process (mabadiliko ni mchakato)
Tunawezaje kushinda bila reforms?
Kikwazo kikuu cha chaguzi huru na za haki hapa nchini, si katiba na sheria mbaya pekee bali ni ukosefu wa utashi wa kisiasa (lack of political will).
Reforms ni muhimu katika kuboresha chaguzi ziwe huru na za haki, lakini reforms pekee, bado haziwezi kuwa muarobaini wa kumaliza vikwazo vyote vya demokrasia. Kikwazo kikuu ni kukosekana kwa utashi wa kisiasa (lack of political will), kunakofanya hujuma na ukandamizaji wa demokrasia uendelee kutamalaki hata pale ambapo katiba na sheria za uchaguzi hazijahalalisha.
Mathalan, si katiba wala sheria zilizopo za uchaguzi zinazohalalisha kuzuiwa kwa mawakala wa vyama vya upinzani kuingia kwenye vituo vya kupigia kura au zinazohalalisha kura feki kuingizwa vituoni; lakini bado yote hayo yanafanyika kinyume kabisa na katiba na sheria zilizopo.
Kwa hiyo, kwa muktadha huo, Chadema inaweza kushinda uchaguzi katika mazingira magumu iwapo itaingia kwenye uchaguzi ikiwa na mkakati kabambe wa ushindi, organaizesheni imara ya nguvu ya umma na raslimali za kutosha kudhibiti hujuma na uhuni mwingi unaofanyika nje kabisa ya mapungufu ya katiba na sheria zilizopo.
G-55
#MawazoMbadala.