Chuo Kikuu cha Dodoma ( UDOM) Kupitia Ndaki ya Insia na Sayansi za Jamii ( CHSS) Idara ya Geografia na Stadi za Mazingira kwa Kushirikiana na na Wakala wa Barabara Tanzania ( TANROADS) Kupitia Mradi wa Jawabu la Ujanishaji ( Green Solutions Project-GSP) tarehe 11 Juni 2025 katika Ukumbi wa Chuo cha VETA- Dodoma wameendesha Warsha maalumu kwa wadau mbalimbali wa mazingira katika Utekelezaji wa Awamu ya kwanza ya Mradi.
Mradi huo, unalenga kuboresha mazingira mbalimbali ambayo yanaharibiwa kutokana na Shughuli mbalimbali za ujenzi wa barabara kama vile upandaji wa miti na Kusaidia serikali katika Kupambana na mabadiliko ya nchi ambapo kwa sasa unatazamia kuboresha mazingira ya ujenzi wa barabara ya mzunguko ( Ring Road Dodoma).
Alizingumza wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo hayo; Mratibu wa Mradi wa Green Solution Project (GSP) kutoka Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Dodoma, Bw. Julius Ruhoro amesema kutokana na ufinyu wa bajeti, ukataji wa miti ovyo na ukosefu wa uandaaji wa kanuni za upandaji wa miti imekuwa changamoto ya kudumu katika utekelezaji wa miradi ya utunzaji wa mazingira jijini humo.