Influencer

Joined June 2009
5,498 Photos and videos
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akifuatilia Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2026/2027, kupitia Televisheni ya Taifa (TBC1), Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 11 Juni, 2026. Bajeti hiyo ilikuwa ikisomwa Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, kwenye Bunge la 13, Mkutano wa tatu katika Kikao cha 48 Jijini Dodoma.
79
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipiga makofi pamoja na Wasaidizi wake mara baada ya Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar kumaliza kuwasilisha Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2026/2027 kwenye Bunge la 13, Mkutano wa tatu katika Kikao cha 48 Jijini Dodoma. Rais Dkt. Samia alikuwa akifuatilia Hotuba ya Bajeti hiyo Kuu ya Serikali kupitia Televisheni ya Taifa (TBC1), Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 11 Juni, 2026.
51
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Massad Boulos, mwanadiplomasia na Mshauri Mwandamizi wa Rais Donald Trump kuhusu masuala ya Afrika, nchi za Kiarabu na Mashariki ya Kati, baada ya kufanya mazungumzo pembezoni mwa Mkutano wa Oslo Forum unaofanyika Oslo, Norway. Mkutano huo, unaofanyika kuanzia tarehe 10 hadi 12 Juni, 2026, umewakutanisha viongozi, wanadiplomasia waandamizi na wadau wa masuala ya amani, diplomasia na usuluhishi kutoka nchi mbalimbali zenye ushawishi duniani. @jmkikwete
81
ASILIMIA 80 MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KUFIKIWA IFIKAPO MWAKA 2034 Naibu Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Salome Makamba (kushoto), akipokelewa na Mshauri Mkuu wa Kiufundi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Bw. Peter Malika, kabla hajazindua Kongamano la Kitaifa siku mbili la Nishati Safi ya Kupikia, lililoanza jijini Arusha leo. Kongamano hilo likiwa na kauli mbiu, "Kuendeleza Mustakabali wa Nishati Safi ya Kupikia Tanzania: Mafanikio, Ushirikiano na Njia za Kufikia Asilimia 80 ya Matumizi ifikapo 2034," linaangazia umuhimu wa kuoanisha sera, ufadhili na mikakati ya ushirikishwaji wa jamii ili kuharakisha maendeleo. Kongamano hilo limeandaliwa na UNCDF kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania, kupitia Wizara ya Nishati, kwa msaada wa Umoja wa Ulaya (EU). Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Nishati Safi ya Kupikia, Wizara ya Nishati, Nolasco Mlay na kulia ni Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Polycarp Nkuyumba
58
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mwigulu Nchemba akimsikiliza Mbunge wa jimbo la Kilindi Mhe.Salehe Mbwana Mhando leo Jumatano Juni 10,2026 bungeni jijini Dodoma.
150
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Kenya Mhe. William Samoei Ruto walipokutana wakati wa mkutano wa Jukwaa la Amani la Oslo 2026 (Oslo Forum 2026) unaofanyika mjini Oslo, Norway, tarehe 10–11 Juni 2026. Mkutano huo wa kimataifa wa kila mwaka unawaleta pamoja wasuluhishi wa migogoro, viongozi wa ngazi za juu, na wataalamu wa amani kutoka zaidi ya nchi 50 duniani. Mwaka huu, Oslo Forum inajadili kauli mbiu yenye uzito wa kipekee: "Gharama ya Vita, Thamani ya Amani" ("The Cost of War, the Price of Peace"). @jmkikwete
1
47
CHAPA MPYA YA MAGARI YA JETOUR YAZINDULIWA TANZANIA WAZIRI wa Viwanda na Biashara Judith Kapinga, amesema Serikali imeendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji na biashara kwa kuboresha sera, sheria na mifumo ya utoaji huduma kuvutia uwekezaji wenye tija. Kapinga ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa chapa mpya ya magari Jetour, jijini Dar es Salaama, ambapo amefafanua uzinduzi huo unaendana kikamilifu na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano na Ajenda ya Taifa ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda na Biashara. Ameongeza uwekezaji huo unadhihirisha dhamira ya kukuza ushiriki wa sekta binafsi, kuongeza matumizi ya rasilimali za ndani,uhamishaji wa teknolojia na kuzalisha ajira kwa Watanzania. "Tunatambua Africarriers na Jetour hawaleti magari pekee nchini bali wanaleta fursa mpya za biashara, uwekezaji, ajira, maarifa ya kiteknolojia na mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania na ukanda wetu wa Afrika Mashariki,”amesema Waziri Kapinga. Pia amewapongeza viongozi wa Africarriers Group na Jetour Global kwa maono yao makubwa kuichagua Tanzania kuwa sehemu ya safari yao ya ukuaji na mafanikio huku akisisitiza Serikali itaendelea kushirikiana na wawekezaji wote wenye nia ya dhati ya kuchangia maendeleo ya Taifa letu. Akieleza zaidi amesema ujio wa Jetour nchini Tanzania kunafungua ukurasa mpya wa fursa za kiuchumi na uwekezaji huo utazalisha ajira mpya kwa vijana katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya mauzo, huduma za kiufundi, ushauri wa huduma kwa wateja, teknolojia ya habari na mawasiliano pamoja na huduma nyingine. Waziri Kapinga amesema pia mafanikio ya Africarriers kwa kipindi cha zaidi ya miaka 50 ni ushahidi wa uwezo, uthubutu na ustahimilivu wa wafanyabiashara wa Kitanzania.
1
104
CHAPA MPYA YA MAGARI YA JETOUR YAZINDULIWA TANZANIA WAZIRI wa Viwanda na Biashara Judith Kapinga, amesema Serikali imeendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji na biashara kwa kuboresha sera, sheria na mifumo ya utoaji huduma kuvutia uwekezaji wenye tija. Kapinga ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa chapa mpya ya magari Jetour, jijini Dar es Salaama, ambapo amefafanua uzinduzi huo unaendana kikamilifu na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano na Ajenda ya Taifa ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda na Biashara. Ameongeza uwekezaji huo unadhihirisha dhamira ya kukuza ushiriki wa sekta binafsi, kuongeza matumizi ya rasilimali za ndani,uhamishaji wa teknolojia na kuzalisha ajira kwa Watanzania. "Tunatambua Africarriers na Jetour hawaleti magari pekee nchini bali wanaleta fursa mpya za biashara, uwekezaji, ajira, maarifa ya kiteknolojia na mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania na ukanda wetu wa Afrika Mashariki,”amesema Waziri Kapinga. Pia amewapongeza viongozi wa Africarriers Group na Jetour Global kwa maono yao makubwa kuichagua Tanzania kuwa sehemu ya safari yao ya ukuaji na mafanikio huku akisisitiza Serikali itaendelea kushirikiana na wawekezaji wote wenye nia ya dhati ya kuchangia maendeleo ya Taifa letu. Akieleza zaidi amesema ujio wa Jetour nchini Tanzania kunafungua ukurasa mpya wa fursa za kiuchumi na uwekezaji huo utazalisha ajira mpya kwa vijana katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya mauzo, huduma za kiufundi, ushauri wa huduma kwa wateja, teknolojia ya habari na mawasiliano pamoja na huduma nyingine. Waziri Kapinga amesema pia mafanikio ya Africarriers kwa kipindi cha zaidi ya miaka 50 ni ushahidi wa uwezo, uthubutu na ustahimilivu wa wafanyabiashara wa Kitanzania.
29
NMB YATANGAZA AWAMU MPYA YA UKUAJI BAADA YA KUREKODI FAIDA YA KODI ZAIDI YA SH TRILIONI MOJA Benki ya NMB imetangaza kuingia katika awamu mpya ya ukuaji baada ya kukamilisha Mpango wake wa Muda wa Kati wa mwaka 2021 hadi 2025, uliowezesha benki hiyo kurekodi faida kabla ya kodi ya zaidi ya Sh1 trilioni na kuongeza mchango wake katika uchumi wa Tanzania. Akizungumza wakati wa mkutano wa wawekezaji jijini Dar es Salaam kuelekea Mkutano Mkuu wa 26 wa Wanahisa, Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, alisema miaka mitano iliyopita imejenga taasisi imara zaidi, yenye mtindo wa biashara wenye ustahimilivu na msingi thabiti wa kuingia katika awamu inayofuata ya ukuaji. Katika kipindi hicho, NMB ilieleza kuwa imeelekeza zaidi ya Sh28 trilioni katika sekta za kimkakati na jumuishi, kwa miaka minne (2021- 2024) imelipa zaidi ya Sh700 bilioni kama gawio kwa wanahisa ( imechangia Sh2.7 trilioni katika kodi na kuwekeza Sh24 bilioni katika miradi ya maendeleo ya jamii. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, alisema taasisi kama NMB zina nafasi muhimu katika kukuza uchumi rasmi, kupanua upatikanaji wa mitaji na kuunga mkono utekelezaji wa Dira 2050, huku NMB ikisema awamu yake ya sasa (Agenda 2030 inalenga zaidi ufadhili endelevu, huduma za kidijitali, huduma bora zaidi kwa wateja na fursa za ukuaji wa kikanda. @NMBTanzania
1
62
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akimpokea mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Singapore, Mhe. Tharman Shanmugaratnam,leo Juni 9,2026 Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi. @samia_suluhu_hassan @ikulu_mawasiliano
1
48
STANDARD CHARTERED YAONGOZA TUKIO LA UPANDAJI MITI BAGAMOYO. Kama sehemu ya dhamira yake ya kukuza uendelevu wa mazingira na uhifadhi wa mazingira, Standard Chartered Tanzania imeongoza shughuli ya upandaji miti katika Shule ya Sekondari Nianjema, Wilaya ya Bagamoyo. Shughuli hiyo inaakisi juhudi zinazoendelea za benki katika kuunga mkono hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kuhamasisha uelewa wa masuala ya mazingira na kuchangia katika uhifadhi wa mifumo asilia ya ikolojia ya Tanzania. Mpango wa mwaka huu una umuhimu wa kipekee kwani unaadhimisha miaka 20 ya kujitolea kwa wafanyakazi wa Standard Chartered, ukiashiria miongo miwili ya hatua za pamoja, mchango kwa jamii na ushiriki wa wafanyakazi katika shughuli za kijamii na kimazingira. Tukio hilo liliwakutanisha wafanyakazi wa benki, viongozi wa eneo husika, wanafunzi na wanajamii katika juhudi za pamoja za kuongeza uoto wa kijani na kuimarisha umuhimu wa utunzaji wa mazingira, Kupitia ushiriki huo, benki inalenga si tu kurejesha mazingira bali pia kuhamasisha utamaduni wa uendelevu kwa vizazi vijavyo. Mpango huo uliongozwa rasmi na wawakilishi wa serikali za mitaa, jambo lililoonesha umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi na kusukuma mbele vipaumbele vya taifa katika masuala ya mazingira. Akizungumza kabla ya tukio hilo, Mkuu wa Transaction Banking Tanzania, Busara Raymond, alisema “Mazingira ni msingi wa uhai wetu ndiyo chanzo cha hewa ya oksijeni tunayopumua, malighafi tunazotegemea na mifumo ya ikolojia inayodumisha maisha. Hii ndiyo sababu uhifadhi wa mazingira ni muhimu sana, na kwa nini Standard Chartered inaendelea kuweka kipaumbele katika mipango inayolinda na kuhifadhi mazingira yetu.” “Huu ni mwaka wetu wa tano mfululizo kupanda miti Bagamoyo, jambo linalodhihirisha dhamira yetu ya muda mrefu kwa jamii hii. Mwaka jana tulipanda miche 2,000 katika Shule ya Msingi Fukayosi, na tunajivunia kuendelea kujenga juu ya mafanikio hayo, Mbali na upandaji miti, tunaendelea kushiriki kikamilifu katika shughuli nyingine za kujitolea kwa jamii, ikiwemo kikao cha hivi karibuni cha ushauri na uongozi kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Pugu Boys.” Tukio hilo pia lilihudhuriwa na Katibu Tawala wa Wilaya (DAS) wa Bagamoyo, jambo lililoonesha ushirikiano imara kati ya sekta ya umma na binafsi katika kuendeleza mipango ya uendelevu wa mazingira. Kupitia ushirikiano huo, benki imefanikiwa kupanda zaidi ya miti 10,000 katika Wilaya ya Bagamoyo pekee na zaidi ya miti 30,000 katika Mkoa wa Dar es Salaam, hatua iliyochangia kuboresha uendelevu wa mazingira na kuunga mkono malengo ya upandaji miti nchini. Kwa miaka mingi, benki imekuwa ikitekeleza programu mbalimbali zinazolenga jamii kwa lengo la kuimarisha ustahimilivu dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi na kuhamasisha maendeleo endelevu.
1
62
UNAWAZO BUNIFU LA KUISAIDIA TRA? ZINGATIA MAENEO HAYA NA UPATE FURSA YA KUSHINDA HADI SHILINGI MILIONI 50, WASHINDI 1020 KUNUFAIKA Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekuletea mashindano ya Wazo Bunifu yanayolenga kupata suluhisho za kibunifu zitakazochangia kuboresha mfumo wa kodi nchini. Hii ni fursa yako ya kuwasilisha wazo lenye tija na kushindania zawadi ya hadi Shilingi Milioni 50. Mawazo yatakayowasilishwa yanapaswa kulenga eneo moja au zaidi kati ya yafuatayo ; kupanua wigo wa kodi, kurahisisha ukadiriaji na ulipaji wa kodi kwa biashara ndogo ndogo, kuimarisha huduma za kodi za kidijitali, kupunguza gharama za ukusanyaji wa mapato, kutumia teknolojia za kisasa kama AI, Big Data na Blockchain katika usimamizi wa kodi, pamoja na kuboresha utatuzi wa migogoro ya kodi ili kuwa wa haraka, wazi na wenye kuaminika zaidi. Tuma wazo lako bunifu kupitia tovuti ya TRA (tra.go.tz) kipengele cha Innovation Portal Ushinde. Mwisho wa kutuma ni Julai 31 , 2026.
1
5
51
TAARIFA KWA UMMA
140
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Rais Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tarehe 06 Juni, 2026 baada ya kuhitimisha Ziara yake ya Kitaifa, St. Petersburg nchini Urusi tarehe 05 Juni, 2026 kufuatia mwaliko wa Rais wa Nchi hiyo Mhe. Vladmir Putin.
1
71
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiagana na viongozi mbalimbali kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam kabla ya kuondoka nchini, kuelekea Shirikisho la Urusi kwa ziara ya Kitaifa itakayoanza tarehe 3 hadi 5 Juni, 2026 kwa mualiko wa Rais wa Shirikisho la Urusi, Mheshimiwa Vladimir Putin
70
RAIS SAMIA KUFANYA ZIARA YA KIHISTORIA NCHINI URUSI
64
WILAYA YA HANANG-MANYARA Katibu wa NEC Itikadi,Uenezi na Mafunzo wa CCM Ndugu Kenani Laban Kihongosi ameanza ziara mkoa wa Manyara kwa kutembelea Mabalozi na kufanya vikao vya shina,Kukagua miradi ya Maendeleo na Kufanya mkutano wa hadhara kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Wilaya ya Hanang mkoani humo.@kenanikihongosi @ccmtanzania #Kazinaututunasongambele #Ziara inaendelea Kesho Babati Mjini.
1
53
JK AKUTANA NA BI. CATHERINE P. CONRAD MINJA, NI MSICHANA ALIYEFANYIWA UPASUAJI WA MOYO KWA MAFANIKIO KATIKA TAASISI YA MIFUPA YA MUHIMBILI (MOI) MIAKA 18 ILIYOPITA Asubuhi ya Ijumaa, Novemba 14, 2008 Rais wa Awamu ya Nne wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, alisimama kwa muda kando ya kitanda cha binti mdogo Catherine P. Conrdad Minja mwenye umri wa miaka minne katika Taasisi ya Mifupa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MOI), akimsabahi na kumtakia nafuu ya haraka baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo mapema wiki hiyo, akiwa mmoja wa wagonjwa wa mwanzo kufanyiwa upasuaji huo katika Taasisi hiyo. Jioni ya Ijumaa Mei 29, 2026 - yaani leo - Rais huyo mstaafu wa Awamu ya Nne wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amekutana kwa mara nyingine na Catherine P. Conrad Minja ambaye Julai 19 mwaka huu atatimiza umri wa miaka 22 , ikiwa ni miaka 18 toka walipoonana katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo mapema wiki hiyo. Catherine hivi sasa ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza akisomea udaktari katika Chuo Kikuu cha Kairuki jijini Dar es salaam, alifika ofisini kwa Rais Mstaafu kumsabahi na kumshukuru kwa juhudi zake za kuanzisha na kusimamia taasisi za magonjwa ya moyo. Dkt. Kikwete amempongeza Catherine kwa kuchagua masomo ya udaktari kama alivyomuahidi miaka 18 iliyopita, na amefurahi kumuona mmoja wa wagonjwa wa kwanza kufanyiwa upasuaji Taasisi ya MOI ambayo ni moja ya taasisi za rufaa zinazoongoza Afrika Mashariki katika kushughulikia kesi ngumu za magonjwa na majeraha ya mifupa, misuli, viungo, ubongo na mfumo wa fahamu. Catherine amemwambia Rais Mstaafu kwamba angependa kuwa Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo huko mbeleni, ili asaidie watu wenye shida hiyo iwe kama shukrani zake kwa Mungu kwa kuwezesha apone na kuendelea kuishi.
6
5
101
16,292
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa kikao cha kupokea Taarifa ya Sensa ya Wanyamapori iliyofanyika nchi nzima mwaka 2024 – 2025 iliyowasilishwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Ashatu Kijaji, tarehe 29 Mei, 2026 Ikulu Dar es Salaam.
2
230
WAZIRI MKUU AKUTANA NA PROF. JANABI BRAZZAVILLE WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika (WHO AFRO), Profesa Mohamed Janabi ambapo walijadili masuala mbalimbali ya maendeleo, hususan ushirikiano katika sekta ya afya barani Afrika. Pia, Dkt. Mwigulu alikutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Balozi Stephen Mbundi pamoja na Katibu Mkuu wa Jukwaa la Mabunge ya Ukanda wa Maziwa Makuu Afrika (FP-ICGLR), Balozi Dkt. Deo Mwapinga. Mazungumzo hayo yamefanyika kando ya Mkutano wa 61 wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), unaoendelea jijini Brazzaville, Jamhuri ya Kongo leo Jumatano Mei 27, 2026.
2
155