Vijana wadogo washajiamulia mambo
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema limewakamata watu wanne wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya mmiliki wa kiwanda cha kuchakata chupa (XIL LI), Bhaozan Li, mwenye asili ya China, ambaye anadaiwa kuuawa na walinzi wake.
Polisi wamesema baada ya mahojiano ya kina, watuhumiwa hao wamekiri kula njama kwa pamoja kumvamia usiku, kumshambulia na baadaye kumuua baada ya kuiba pesa TZS milioni 9 zilizokuwa ndani ya kiwanda.