gaditvOnline-Ukurasa huu unahusika na kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha. Karibu msomaji na mtazamaji wetu, hapa utakutana na habari za Siasa, Kijamii nk.
"Ikiwa unatafuta mtu anayejua kitu kuhusu vita, tafadhali njoo kwangu. Ninajua kitu juu yake na najua jinsi ilivyo mbaya. Na kwa hilo, najua jinsi huwezi kuwa na kitu bora zaidi kuliko amani." Rais wa Rwanda Paul Kagame.
Picha ya mnato ambayo imepigwa na GADI TV ikionesha Mzoga wa Ng'ombe unayedaiwa kufa ghafla ukiwa unachunwa kwenye kijiji cha Sekei kata ya Kiutu Wilayani Arumeru, kwa ajili ya kwenda kuuzwa kwa baadhi ya bucha na kwa watu wanaouza supu na mishkaki.
Kwa mujibu vyanzo vyetu vimetueleza mizoga ya aina hiyo hugongwa mihuri feki na kufichwa bafuni na kusafirishwa kwenye baadhi ya maeneo ya Mianzini, Sanawari na Ngulelo, wakati wa usiku.
"Mama Samia utaokoa sana hii nchi, tunakuombea utufikishe mwaka 2030, nina hakika wakati huo watakubali haya yote unayoyafanya" Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye.
"Hatuwezi kutisha viongozi, kilimo hakitatuliwi kwakutisha, matatizo ya kilimo yanaondoka kwakujadiliana, na Rais wa awamu ya sita ameonyesha njia ya majadiliano" Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe
"...mlio karibu naye [Bashiru Ally] mwambieni aombe radhi na kisha ajiuzulu! Amepuyanga mno kumsema Rais na mfumo mzima kwa hoja za kichochezi zisizo na ushahidi" Dkt. Hamisi Kigwangalla Mbunge wa Nzega.
"Nimetumiwa malalamiko mengi na wananchi kuwa baadhi ya ving’amuzi nchini vimeondoa channel ya TBC wakati leo wakianza kuonyesha mashindano ya Kombe la Dunia. Nimewaagiza TCRA kushughulikia. Naomba utulivu wakati tukifuatilia jambo hili." Waziri wa Habari, Nape Nnauye
Meneja wa kiwanja cha Ndege cha Arusha, Mhandisi Elipigi Tesha amesema Ndege zinashindwa kutua nyakati za usiku katika uwanja huo kutokana na kukosekana kwa taa za kuongozea Ndege kwenye eneo hilo.
Aidha, kwa upande wa Naibu Waziri wa Uchukuzi Bw. Atupele Mwakibete akijibu chanagamoto hiyo ya ukosefu wa taa katika eneo hilo, amesema itatuliwa katika mwaka wa fedha ujao.
Diwani wa kata ya Kawe Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Muta Rwakatare inadaiwa kuwa amepotea kwa miezi kadhaa ikiwa mara ya pili baada ya tukio la kwanza la kupotea na kupatikana kwa Ashura Ally mnamo Mei 24 mwaka huu eneo la Tabata.
Watu sita waliokuwa wakisafiria gari la kubeba wagonjwa (Ambulance) wilaya ya Kiteto mkoani Manyara wamefariki dunia baada ya gari hilo kugongana na Prado usiku wa kuamkia leo Novemba 8, 2022 eneo la Pori namba moja.
Aneth Kaaya aliyefariki dunia kufuatia ajali ya ndege ya Precision Air katika ziwa Victoria, familia yake imesema Aneth alikuwa akisafiri kuelekea Bukoba kwa ajili ya kutambulishwa ukweni.
Kijana ambaye amekuwa maarufu nchini kwa kuokoa watu 23 kwenye ajali ya ndege ziwa Victoria, Majaliwa Jackson ambaye pia Rais Samia ameagiza aingizwe kwenye jeshi la uokoaji, akiwa amemkumbatia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa zoezi la kuaga miili ya watu 19, Novemba 7, 2022
Rais Samia ameagiza kijana Majaliwa (Mvuvi) aliyeshiriki kuokoa abiria kwenye ajali ya dege Bukoba akabidhiwe kwa Waziri wa mambo ya ndani na atafutiwe nafasi kwenye jeshi la uokozi ili kijana huyu apate mafunzo zaidi ya ujasiri zaidi.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Jambo For Development, Bi Imani Paulo ni miongoni mwa watu 19 waliofariki dunia kufuatia ajali ya ndege ya Precision Air PW-494 katika ziwa Victoria Novemba 6, 2022.
Wanaume wawili wanaoshukiwa kuwa wezi wa ng'ombe Nchini Kenya wamejisalisha mikononi mwa polisi nchini humo wakiwa na ng'ombe aliyedaiwa kuibwa huku mmoja wao akiwa na bunda la nyuki viganjani mwake akionekana kuwa na maumivu makali.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa amembeba mtoto Emly Victor (1.4) aliyenusurika kifo pamoja na mama yake katika ajali ya ndege ya Precisian Air iliyotokea ziwa Victoria mkoani Kagera leo Novemba 6, 2022.