"Sio tu Jimbo langu, majimbo yote ya Dar es Salaam wananchi wanalalamikia barabara, Serikali inafanyeje? Inakwenda Benki ya Dunia, inachukua mkopo Dola Mil. 438 karibu Tril. 1.2 inajengwa mradi wa Dar es salaam Metropolitan Development Project (DMDP) awamu ya pili ambao ni mradi maarufu sana Dar es Salaam.
Mradi ule ukikamilika mtu wa Bombambili, Majohe ambaye alikuwa akitumia Tshs 2,000 kufika Mombasa, Ukonga na kutumia Saa Tatu kufika Kariakoo, atatumia Tshs 700 kutoka Bombambili- Kariakoo na hali ya maisha itaongezeka na Pato la Taifa litaongezeka"- Jerry Silaa - Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
@jerrysilaa
#PBCloudsFM
#GenCForLife