📺 𝗞𝘄𝗲𝗻𝘆𝗲 𝗞𝗧𝗡: 𝗞𝘂𝗲𝗹𝗶𝗺𝗶𝘀𝗵𝗮 𝗨𝗺𝗺𝗮 𝗞𝘂𝗵𝘂𝘀𝘂 𝗦𝗮𝗿𝗮𝘁𝗮𝗻𝗶 𝘆𝗮 𝗦𝗵𝗶𝗻𝗴𝗼 𝘆𝗮 𝗞𝗶𝘇𝗮𝘇𝗶 𝗻𝗮 𝗨𝗽𝗶𝗺𝗮𝗷𝗶 𝘄𝗮 𝗛𝗣𝗩 📣
Wiki hii, Jumanne tarehe 21/01/2026, nilipata fursa ya kuwa kwenye runinga ya KTN, ambapo nilizungumza kuhusu saratani ya shingo ya kizazi (cervical cancer) - moja ya saratani zinazoathiri wanawake wengi lakini inaweza kuzuilika na kugunduliwa mapema.
Saratani hii inasababishwa na virusi vya HPV, ambavyo ni rahisi kupima maabara 🦠
Wanawake wanaopatikana na HPV hufuatiliwa kwa kina, ikiwemo colposcopy, ili kutibu dalili za mapema za chembechembe za saratani 🔬
Upimaji wa HPV kwa kujichukulia sampuli mwenyewe (HPV self-sample collection) ni njia rahisi, salama, ya faragha na isiyo na maumivu, inayomwezesha mwanamke kujipima mwenyewe bila kwenda hospitalini au zahanati.
Ujumbe wangu kwa wanawake wote:
✔️ Pima mapema. Jua hali yako. Jilinde. Jipende. Saratani ya shingo ya kizazi inaweza kuzuilika
💉 Kwa wasichana wa miaka 9–14, chanjo ya HPV inazuia saratani kutokana na HPV watakapoanza maisha ya ndoa.
Asanteni KTN News Kenya kwa jukwaa hili muhimu la kuelimisha umma tukiendelea kushirikiana kuhakikisha wanawake wengi zaidi wanapata taarifa sahihi kuhusu
#HPVTesting na huduma za kisasa za uchunguzi.
🎥 Tazama mahojiano kamili hapa:
youtu.be/9YJe4T4Ak-E?si=Qz8l…
***************************
📺 𝗢𝗻 𝗞𝗧𝗡: 𝗘𝗱𝘂𝗰𝗮𝘁𝗶𝗻𝗴 𝘁𝗵𝗲 𝗣𝘂𝗯𝗹𝗶𝗰 𝗼𝗻 𝗖𝗲𝗿𝘃𝗶𝗰𝗮𝗹 𝗖𝗮𝗻𝗰𝗲𝗿 𝗮𝗻𝗱 𝗛𝗣𝗩 𝗧𝗲𝘀𝘁𝗶𝗻𝗴 📣
This week, on Tuesday 21/01/2026, I had the opportunity to appear on KTN television, where I spoke about cervical cancer — one of the cancers that affects many women, yet is preventable and can be detected early.
This cancer is caused by the HPV virus, which is easy to test for in the laboratory 🦠
Women who test positive for HPV are closely followed up, including with procedures such as colposcopy, to treat early precancerous changes 🔬
HPV self-sample collection is a simple, safe, private, and painless method that allows a woman to collect her own sample without having to visit a hospital or clinic.
My message to all women:
✔️ Test early. Know your status. Protect yourself. Love yourself. Cervical cancer is preventable.
💉 For girls aged 9–14 years, the HPV vaccine prevents HPV-related cancers later in life when they begin marital life.
Thank you, KTN News Kenya, for this important platform to educate the public as we continue to work together to ensure more women receive accurate information on
#HPVTesting and modern screening services.
🎥 Watch the full interview here:
youtu.be/9YJe4T4Ak-E?si=Qz8l…