Filter
Exclude
Time range
-
Near
STAMIGOLD YAANDIKA HISTORIA YAONGEZA UHAI WA MGODI HADI 2032 ● Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini yaipongeza kwa uwekezaji wa mitambo ya kisasa ● Yatajwa kurefusha uhai wa mgodi kwa miaka sita zaidi kupitia ugunduzi wa mashapo mapya ● Yatoa ajira 740 kwa wazawa, yagundua akiba mpya ya wakia 100,319 📍Biharamulo KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeipongeza Kampuni ya Uzalishaji Dhahabu ya STAMIGOLD inayosimamiwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), kufuatia mafanikio makubwa ya uzalishaji wa dhahabu na kurefusha uhai wa mgodi hadi mwaka 2032. Pongezi hizo zilitolewa Juni 13, 2026 na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Subira Mgalu, wakati wa ziara maalum ya wajumbe wa kamati hiyo iliyolenga kukagua shughuli za uzalishaji madini katika mgodi huo uliopo wilayani Biharamulo. Kufuatia hatua hiyo, Mhe. Mgalu aliitaka STAMICO kuendelea kufanya utafiti wa kina katika maeneo ya leseni zake zilizotengwa ili kupata taarifa mpya zitakazowezesha kuanzisha mgodi mwingine mpya wa dhahabu ili kuendelea kuimarisha kampuni ya STAMIGOLD. Pia, alishauri STAMICO kuendeleza uwekezaji katika sekta ya madini kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo hususan kwenye utafiti wa madini mkakati ili kuongeza idadi ya migodi itakayosaidia katika maendeleo ya uchumi kwa taifa. Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, aliishukuru Kamati ya Bunge kwa ushauri wake wa kiufundi na kubainisha kuwa Wizara ya Madini itaendelea kupokea maoni na ushauri huo ili kuendeleza sekta, hususan kwenye maeneo ya ushirikiano wa kimkakati katika uwekezaji kupitia taasisi zake za utendaji. Naye, Mkurugenzi Mkuu wa STAMICO, Dkt. Venance Mwase, alieleza kuwa mgodi unaendelea na uhakiki pamoja na utafiti ndani ya leseni maalum ya uchimbaji kwa kutumia njia mbalimbali za ukusanyaji wa taarifa na ukadiriaji upya ili kuongeza taarifa za akiba ya mashapo ya mgodi huo. Awali, akiwasilisha taarifa ya utendaji ya kampuni hiyo, Meneja Mkuu wa Mgodi wa STAMIGOLD Ali Ali alisema kuwa kuanzia mwezi Julai 2014 hadi Mei 2026, jumla ya wakia 137,049.73 za dhahabu zimezalishwa. Ali aliongeza kuwa, mgodi umefanikiwa kuongeza ufanisi kwa kununua mtambo mkubwa wa kisasa wa uchorongaji unaopunguza gharama za uendeshaji, pampu kubwa za kusukuma maji migodini, pamoja na kufanikiwa kutoa ajira za muda mfupi na mrefu kwa wazawa 740.
4
84
🚀 STAMIGOLD Extends Mine Life to 2032 Through New Gold Discoveries and Strategic Investment🇹🇿 A major milestone for Tanzania’s mining sector. During a visit by the Parliamentary Standing Committee on Energy and Minerals, STAMIGOLD under the stewardship of State Mining Corporation (STAMICO) received commendation for its strong operational performance, investment in modern mining technology, and successful resource expansion. 🔹 Mine life extended by six additional years, now projected to operate until 2032 🔹 Discovery of 100,319 ounces of new gold reserves 🔹 Production of over 137,000 ounces of gold since 2014 🔹 Employment opportunities created for 740 Tanzanians 🔹 Investment in advanced drilling equipment and mine dewatering systems to improve efficiency and reduce operational costs The achievement demonstrates how continuous exploration, technological innovation, and strategic investment can unlock long-term value in the mining industry while creating jobs and contributing to national economic growth. As Tanzania advances its ambitions under Vision 2050, success stories such as STAMIGOLD highlight the critical role of resource development, local participation, and sustainable mining in driving industrialization and shared prosperity. #Mining #TanzaniaMining #STAMIGOLD #STAMICO #GoldMining #MineralDevelopment #Investment #EconomicGrowth #MiningInnovation #SustainableMining #Vision2050 #Tanzania #NaturalResources #MiningIndustry ⛏️🇹🇿✨
2
4
170
and sustainable mineral economies. 📺 Watch now and join the conversation. 🔔 Subscribe for more insights on Africa’s energy and extractives sector. #Mining #Tanzania #STAMICO #EastAfrica #Minerals #Investment #Industrialization #Extractives
23
Africa’s mining sector is increasingly becoming a driving force for industrialization, economic growth, and regional transformation. In this insightful episode, we explore the strategic role that STAMICO is playing in shaping the future of Tanzania’s mining industry.
1
1
2
40
🔔 Subscribe to Everything Energy & Extractives and stay connected to the leaders, ideas, and innovations shaping the future of energy and mining in Africa. #EverythingEnergyAndExtractives #STAMICO #UCEM
2
4
162
🎙️ NEW EPISODE | EVERYTHING ENERGY & EXTRACTIVES Africa's mining sector continues to emerge as a catalyst for industrialization, economic transformation, and regional development. In this insightful episode, we discuss the pivotal role STAMICO is playing in shaping Tanzania's mining future. Discover how #Tanzania is positioning itself as a leading mining destination, the opportunities available for investors and industry players, and why stronger partnerships within #EastAfrica are critical to building resilient and competitive mineral economies. 📺 Tune in 🔔 Subscribe #EverythingEnergyAndExtractives #STAMICO #UCEM
3
8
315
🎙️ New Episode Alert! #EverythingEnergyandExtractivesPodcast Join our CEO @humfas, in conversation with Dr. Venance B. Mwasse, Managing Director of @STAMICOTZ, as they explore how the State Mining Corporation is driving Tanzania’s mining transformation and unlocking new opportunities for growth, investment, and regional collaboration. ⛏️ Topic: STAMICO at the Forefront of Tanzania’s Mining Growth #Subscribe to Everything Energy & Extractives and be part of the conversations shaping Africa’s resource future. #STAMICO #UCEM
3
8
192
UPDATE: STAMICO: Dr. Venance Mwasse anaendela; Amb. Said Yakub ni Naibu Waziri @mfa_tanzania kachukua nafasi ya Elsie Kanza,Eng. Rogatus Mativila Katibu Mkuu Ujenzi. @ikulumawasliano @NPC_Tanzania @jwtztaarifa @gcumod @UKinTanzania @bunge_tz @RoyalNavy @RoyalMarines @BritishArmy
70
ضربة معلم استثمارية جديدة لقطر في أفريقيا! 🇶🇦🤝🇹🇿 امس، شهدت الدوحة توقيع اتفاقية تعدين استراتيجية ضخمة بين شركة "Thirty-Five Holding" ومؤسسة التعدين التنزانية (STAMICO). الشراكة بتركز على استخراج ومعالجة 3 موارد حيوية (الذهب، النحاس، والمعادن النادرة) لتأمين تكنولوجيا المستقبل، مع دعم وتأهيل آلاف المعدّنين الصغار هناك ....
1
11
38
4,282
TANZANIA, QATAR ZAFUNGUA FURSA MPYA SEKTA YA MADINI 🇶🇦 🇹🇿 ✅Al Mansour Group Yaonesha Nia Kuwekeza kwenye Uongezaji Thamani wa Dhahabu, Nikeli, Kobalti na Chuma ✅Teknolojia, Mitambo, Mafunzo na Uzalishaji wa Mbolea Vyatajwa Maeneo Muhimu ya Ushirikiano ✅Wachimbaji Wadogo Waguswa 📍 Doha, Tanzania imeendelea kupanua wigo wa ushirikiano wa kimataifa katika Sekta ya Madini baada ya Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Madini ikiongozwa na Kamishina Msaidizi wa Madini anayesimamia Uongezaji Thamani wa Madini, Mhandisi Modest Apolinary, kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Al Mansour Group, Mhe. Sheikh Mansour Bin Jabour Bin Jassim Al Thani, ambaye pia ni Mwanafamilia wa Kifalme wa Qatar. Mazungumzo hayo yaliyofanyika Juni 1, 2026 yalilenga kujadili fursa za uwekezaji na maeneo ya ushirikiano katika Sekta ya Madini nchini Tanzania, ikiwa ni mwendelezo wa jitihada za Serikali za kuvutia uwekezaji wa kimkakati kufuatia ziara ya Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, aliyoifanya nchini Qatar mwezi Februari 2026. Katika kikao hicho, pande zote mbili zilijadili fursa mbalimbali za uwekezaji katika mnyororo wa thamani wa madini, hususan madini muhimu na ya kimkakati. Kampuni ya Al Mansour Group ilionesha nia ya kuwekeza katika shughuli za uongezaji thamani wa madini ya dhahabu, nikeli, kobalti na chuma, hatua inayokwenda sambamba na mkakati wa Tanzania wa kuongeza thamani ya rasilimali zake kabla ya kuuzwa katika masoko ya kimataifa. Majadiliano hayo pia yalihusisha uwezekano wa ushirikiano katika utengenezaji na usambazaji wa mitambo pamoja na vifaa vinavyotumika katika shughuli za utafiti, uchorongaji, uchimbaji na uchenjuaji wa madini. Kutokana na dhamira hiyo, ilikubaliwa kuwa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) lifanye tathmini ya mahitaji ya wachimbaji wadogo ili kubaini aina ya vifaa vinavyohitajika kwa lengo la kuimarisha shughuli za utafiti na uchimbaji nchini. Aidha, pande hizo mbili zilijadili fursa za ushirikiano katika mafunzo na kubadilishana uzoefu kwa wataalamu wa sekta ya madini, hususan katika maeneo ya utafiti wa madini, teknolojia za uchorongaji, usimamizi wa miradi na elimu ya fedha. Ushirikiano huo unatarajiwa kuongeza uwezo wa kitaalamu na kuimarisha ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya madini nchini. Katika hatua nyingine, majadiliano yaligusia uwekezaji katika uzalishaji wa mbolea kwa kutumia malighafi zinazopatikana Tanzania. Hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mbolea, kupunguza gharama za uzalishaji kwa wakulima na kuchangia ukuaji wa sekta ya kilimo pamoja na kuimarisha usalama wa chakula nchini. Akizungumza katika kikao hicho, Mhandisi Modest Apolinary alisema Wizara ya Madini ipo tayari kushirikiana na Al Mansour Group katika maeneo mbalimbali ya utafiti, uchimbaji, uongezaji thamani wa madini na maendeleo ya rasilimali watu ili kuhakikisha pande zote zinanufaika na ushirikiano huo. Kwa upande wake, Balozi wa Tanzania nchini Qatar, Mhe. Habibu Mohamed, alisema Tanzania inaendelea kuwa miongoni mwa maeneo bora ya uwekezaji kutokana na mazingira yake tulivu, sera rafiki za uwekezaji na mifumo ya kisheria inayolinda mitaji ya wawekezaji. ‘’Tunaikaribisha Al Mansour Group kuwekeza nchini Tanzania na kutumia fursa mbalimbali zilizopo katika Sekta ya Madini, Viwanda na Kilimo,” alisema Balozi Habibu. Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dkt. Venance Mwasse, alisema shirika hilo liko tayari kushirikiana na kampuni hiyo katika maeneo yote ambayo imeonesha nia ya kuwekeza, akibainisha kuwa ushirikiano huo utaongeza uwekezaji, kuhamasisha matumizi ya teknolojia za kisasa, kuimarisha shughuli za utafiti na uchimbaji wa madini pamoja na kuongeza mchango wa sekta ya madini katika uchumi wa taifa. Mazungumzo hayo ya wataalam kutoka Wizara ya Madini, STAMICO na kampuni hiyo yanaashiria hatua mpya katika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Qatar, huku yakifungua fursa za uwekezaji, teknolojia na uongezaji thamani wa rasilimali madini.
5
6
495
WAZIRI MAVUNDE AZINDUA KIWANDA CHA KUCHAKATA CHUMVI WILAYANI KILWA-LINDI ● Atangaza neema kwa wavunaji wa chumvi nchini Tanzania, ● Kiwanda hicho ni utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais ya utatuzi wa changamoto ya soko la chumvi kwa wachimbaji wadogo, ● Zaidi ya tani 25,000 za chumvi kuchakatwa kwa Mwaka, ● Waziri Mavunde aitaka STAMICO kuongeza viwanda zaidi vya kuchakata madini *Kilwa, Lindi* Kufuatia changamoto kubwa ya ukosefu wa soko la chumvi ghafi, Waziri wa Madini *Mhe. Anthony Mavunde (Mb)* ametangaza neema kwa wavunaji wa chumvi baada ya kuzindua kiwanda cha kuchakata chumvi kilichojengwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ambacho kinakwenda kuleta uhakika wa soko la chumvi ya wavunaji wadogo. Mhe. Mavunde ameyasema hayo leo tarehe 29 Mei, 2026 katika eneo la Lingaula, Kilwa Mkoani Lindi alipokuwa akizindua kiwanda cha chumvi cha STAMICO. "*Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan* alitupa maelekezo ya kuhakikisha tunatatua changamoto ya ukosefu wa soko la uhakika wa chumvi ghafi ya wachimbaji wadogo, kero aliyopewa alipofanya ziara Mkoani Lindi" "Leo tupo hapa kipekee kutangaza rasmi kuwa tumetekeleza maelekezo ya Mhe. Rais kwa vitendo. Shirika letu la Madini STAMICO limeleta kiwanda hiki hapa ili kiwe soko la uhakika la wavunaji wetu na kuondokana na kero ya ukosefu wa soko iliyowakabili kwa muda mrefu" alieleza Mhe. Mavunde. Pia, Waziri Mavunde amebainisha kuwa kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuchakata tani 3 kwa saa na hivyo kupelekea kuwa na uwezo wa kuzalisha kati ya tani 15,000 na 25,000 kwa mwaka, na kuwataka wavunaji wa chumvi kuchangamkia fursa hiyo ya uwepo wa soko la uhakika wa chumvi yao. Vilevile, aliigiza STAMICO kuhakikisha inajenga viwanda zaidi vya kuongeza thamani madini nchini kama Sera ya Madini inavyoelekeza. Katika hatua nyingine, Mhe. Mavunde ameeleza kuwa atashirikiana na Waziri wa Viwanda na Biashara ili kuhakikisha chumvi inayozalishwa na wavunaji ndani ya nchi inapata soko la uhakika na inakidhi mahitaji yetu na kuondokana na utegemezi kuagiza chumvi kutoka nje ya nchi. Awali, akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la STAMICO, CPA Dkt. Venance Mwasse amesema ujenzi wa mradi huo utagharimu Shilingi bilioni 4.5 mpaka utakapokamilika na wanataraji si tu kuwa soko la chumvi, bali kuwa kituo mahiri cha mafunzo kwa wavunaji wa chumvi ili waweze kuzalisha chumvi yenye ubora na hatimaye kupata bei nzuri zaidi. Akitoa salamu za wazalishaji wa chumvi, Mwenyekiti wa Chama cha Wazalishaji wa Chumvi Tanzania (TASPA), Bi. Hawa Ghasia ameishukuru Serikali kwa kusikia kilio chao na kuahidi kuwa kiwanda hicho wanakiona kama chao na si cha STAMICO hivyo watahakikisha wanashikiriana nacho ili kuzalisha chumvi yenye ubora unaohitajika kwa walaji. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mheshimiwa Subira Mgalu aliishukuru Serikali kwa kutatua changamoto za wananchi kwa vitendo na kuahidi kuendelea kuisimamia Serikali ili ahadi zake zote zitekelezwe na kuleta tija kwa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi. Naye, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, *Mheshimiwa Zainabu Telack* alionesha kufurahishwa na ujio wa kiwanda hicho na kuahidi kuendelea kushirikiana na STAMICO katika kuhakikisha changamoto ya ukosefu wa soko la chumvi inayozalishwa na wavunaji wadogo inatatuliwa ipasavyo.
3
180
WAZIRI MAVUNDE AZINDUA KIWANDA CHA KUCHAKATA CHUMVI WILAYANI KILWA-LINDI ● Atangaza neema kwa wavunaji wa chumvi nchini Tanzania, ● Kiwanda hicho ni utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais ya utatuzi wa changamoto ya soko la chumvi kwa wachimbaji wadogo, ● Zaidi ya tani 25,000 za chumvi kuchakatwa kwa Mwaka, ● Waziri Mavunde aitaka STAMICO kuongeza viwanda zaidi vya kuchakata madini *Kilwa, Lindi* Kufuatia changamoto kubwa ya ukosefu wa soko la chumvi ghafi, Waziri wa Madini *Mhe. Anthony Mavunde (Mb)* ametangaza neema kwa wavunaji wa chumvi baada ya kuzindua kiwanda cha kuchakata chumvi kilichojengwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ambacho kinakwenda kuleta uhakika wa soko la chumvi ya wavunaji wadogo. Mhe. Mavunde ameyasema hayo leo tarehe 29 Mei, 2026 katika eneo la Lingaula, Kilwa Mkoani Lindi alipokuwa akizindua kiwanda cha chumvi cha STAMICO. "*Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan* alitupa maelekezo ya kuhakikisha tunatatua changamoto ya ukosefu wa soko la uhakika wa chumvi ghafi ya wachimbaji wadogo, kero aliyopewa alipofanya ziara Mkoani Lindi" "Leo tupo hapa kipekee kutangaza rasmi kuwa tumetekeleza maelekezo ya Mhe. Rais kwa vitendo. Shirika letu la Madini STAMICO limeleta kiwanda hiki hapa ili kiwe soko la uhakika la wavunaji wetu na kuondokana na kero ya ukosefu wa soko iliyowakabili kwa muda mrefu" alieleza Mhe. Mavunde. Pia, Waziri Mavunde amebainisha kuwa kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuchakata tani 3 kwa saa na hivyo kupelekea kuwa na uwezo wa kuzalisha kati ya tani 15,000 na 25,000 kwa mwaka, na kuwataka wavunaji wa chumvi kuchangamkia fursa hiyo ya uwepo wa soko la uhakika wa chumvi yao. Vilevile, aliigiza STAMICO kuhakikisha inajenga viwanda zaidi vya kuongeza thamani madini nchini kama Sera ya Madini inavyoelekeza. Katika hatua nyingine, Mhe. Mavunde ameeleza kuwa atashirikiana na Waziri wa Viwanda na Biashara ili kuhakikisha chumvi inayozalishwa na wavunaji ndani ya nchi inapata soko la uhakika na inakidhi mahitaji yetu na kuondokana na utegemezi kuagiza chumvi kutoka nje ya nchi. Awali, akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la STAMICO, CPA Dkt. Venance Mwasse amesema ujenzi wa mradi huo utagharimu Shilingi bilioni 4.5 mpaka utakapokamilika na wanataraji si tu kuwa soko la chumvi, bali kuwa kituo mahiri cha mafunzo kwa wavunaji wa chumvi ili waweze kuzalisha chumvi yenye ubora na hatimaye kupata bei nzuri zaidi. Akitoa salamu za wazalishaji wa chumvi, Mwenyekiti wa Chama cha Wazalishaji wa Chumvi Tanzania (TASPA), Bi. Hawa Ghasia ameishukuru Serikali kwa kusikia kilio chao na kuahidi kuwa kiwanda hicho wanakiona kama chao na si cha STAMICO hivyo watahakikisha wanashikiriana nacho ili kuzalisha chumvi yenye ubora unaohitajika kwa walaji. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mheshimiwa Subira Mgalu aliishukuru Serikali kwa kutatua changamoto za wananchi kwa vitendo na kuahidi kuendelea kuisimamia Serikali ili ahadi zake zote zitekelezwe na kuleta tija kwa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi. Naye, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, *Mheshimiwa Zainabu Telack* alionesha kufurahishwa na ujio wa kiwanda hicho na kuahidi kuendelea kushirikiana na STAMICO katika kuhakikisha changamoto ya ukosefu wa soko la chumvi inayozalishwa na wavunaji wadogo inatatuliwa ipasavyo.
2
9
1,443
🇹🇿 Transforming Tanzania’s Salt Industry Through Value Addition and Market Access✨️ Today marks a significant milestone in Tanzania’s industrialization and mineral value-addition agenda as the Minister of Minerals, Hon. Anthony Mavunde, officially inaugurated STAMICO’s Salt Processing Plant in Kilwa, Lindi. The plant is a direct response to the vision of H.E. President Dr. Samia Suluhu Hassan, who directed the Government to address the long-standing challenge of unreliable markets for raw salt produced by small-scale harvesters. 🔹 Processing capacity of 3 tonnes per hour 🔹 Annual production of 15,000–25,000 tonnes of processed salt 🔹 Total project investment of approximately TZS 4.5 billion 🔹 Creation of a reliable market for small-scale salt producers 🔹 Promotion of local value addition and reduced dependence on imported salt Beyond processing, the facility will serve as a center for training and technology transfer, empowering producers to improve quality, increase competitiveness, and unlock greater economic value from Tanzania’s abundant salt resources. This achievement demonstrates how strategic government leadership, state-owned enterprises, and local producers can work together to strengthen domestic industries, create jobs, and advance Tanzania’s journey toward a more resilient and industrialized economy. #MiningForDevelopment #ValueAddition #Industrialization #TanzaniaMining #SaltIndustry #STAMICO #MineralsSector #MadeInTanzania #EconomicTransformation #SamiaSuluhuHassan #AnthonyMavunde #Lindi #Kilwa
1
9
514
🇹🇿 Transforming Tanzania’s Mining Sector Through Inclusion, Formalization & Accountability✨️ The Government of Tanzania continues to strengthen the mining sector by expanding opportunities for small-scale miners and advancing long-standing commitments to former workers in the industry. ⛏️📈 Speaking in Parliament today, Deputy Minister for Minerals, Steven Kiruswa announced that the Government has officially allocated the Nyakafulu area in Mbogwe District, Geita Region, for small-scale mining activities and issued 108 mining licenses after revoking undeveloped licenses. This strategic intervention reflects a broader national agenda focused on: ✔️ Formalizing small-scale mining ✔️ Expanding economic participation for citizens ✔️ Creating employment opportunities ✔️ Enhancing responsible mineral resource development ✔️ Improving investment efficiency in the sector The Government also revealed that legal assessments are ongoing for 63 underutilized prospecting licenses, with the aim of reallocating viable areas to small-scale miners where appropriate. In another significant development, the Government confirmed that it is finalizing verification processes for compensation claims involving former employees of the Kiwira Mine. Following extensive audits and reviews, verified claims and supplier debts totaling TSh 1.52 billion have already been incorporated into the Government’s debt framework pending final clearance for payment. These developments demonstrate continued efforts toward building a more inclusive, transparent, and sustainable mining industry in Tanzania. 🇹🇿✨ #Mining #Tanzania #SmallScaleMining #Investment #EconomicDevelopment #Minerals #MiningSector #AfricaMining #STAMICO #Sustainability #Leadership #Development #Geita #MiningIndustry
3
7
200
Serikali Yaendelea Kutenga Maeneo Mapya kwa Wachimbaji Wadogo, Leseni 108 Zatolewa ✔️Deni la Bilioni 1.52 la Waliokuwa Wafanyakazi wa Kiwira Kulipwa Baada ya Uhakiki wa Mwisho 📍Dodoma,– Serikali imeendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji na ushiriki wa wananchi katika Madini kwa kuendelea kutenga maeneo maalum kwa ajili ya wachimbaji wadogo nchini, hatua inayolenga kuongeza fursa za ajira, kuinua uchumi wa wananchi na kurasimisha shughuli za uchimbaji mdogo. Katika utekelezaji wa hatua hiyo, Serikali tayari imetenga eneo la Nyakafulu, Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita kwa wachimbaji wadogo na kutoa leseni 108 baada ya kufutwa kwa leseni zilizokuwa haziendelezwi ipasavyo. Hatua hiyo imebainishwa bungeni leo Mei 26, 2026 na Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Dkt. Steven Kiruswa kwa niaba ya Waziri wa Madini wakati akijibu maswali ya wabunge kuhusu maendeleo ya Sekta ya Madini. Akijibu swali la Mbunge wa Mbogwe, Mhe. Fagason Nkingwa aliuliza kuwa ni lini Serikali itatenga maeneo kwa wachimbaji wadogo na kuwapatia leseni za uchimbaji, Dkt. Kiruswa amesema Serikali tayari imetenga eneo la Nyakafulu kwa ajili ya wachimbaji wadogo na kutoa jumla ya leseni 108 baada ya kufutwa kwa leseni ambazo hazikuwa zimeendelezwa. Amesema kuwa, hatua hiyo inaakisi dhamira ya Serikali ya kuendelea kurasimisha na kukuza shughuli za uchimbaji mdogo nchini ili wananchi wengi zaidi waweze kushiriki katika uchumi wa madini kwa tija na manufaa mapana. “Serikali kupitia Tume ya Madini inaendelea kufanya tathmini ya kisheria ya leseni 63 za utafiti ambazo hazijaendelezwa ipasavyo kwa lengo la kuzifuta pale inapobidi na kuyatenga baadhi ya maeneo hayo kwa wachimbaji wadogo,” amesema Dkt. Kiruswa. Aidha, Dkt. Kiruswa ameeleza kuwa Serikali itaendelea kuchambua taarifa za jiosayansi ili kubaini maeneo yenye tija kwa wachimbaji wadogo, huku Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ikipewa jukumu la kufanya tafiti za kina kwenye maeneo yenye taarifa hafifu kabla ya kutengwa rasmi kwa shughuli za uchimbaji mdogo. Katika hatua nyingine, Serikali imeeleza kuwa ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha uhakiki wa madai ya waliokuwa watumishi wa Mgodi wa Kiwira kabla ya kuanza kulipa madeni hayo. Akijibu swali la Mbunge wa Kyela, Mhe. Baraka Mwamengo kuhusu lini Serikali itawalipa waliokuwa watumishi wa Mgodi wa Kiwira, Dkt. Kiruswa ameeleza madai hayo yalitokana na malalamiko ya mapunjo ya mafao kwa wafanyakazi waliokuwa wakihudumu mgodini hapo kabla ya ubinafsishaji. Amefafanua kuwa baada ya malalamiko kuwasilishwa na Chama cha Wafanyakazi Migodini na Ujenzi (TAMICO), Serikali ilifanya ukaguzi maalum kupitia Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mwaka 2008 na baadaye kufanya uhakiki mwingine mwaka 2015. Kwa mujibu wa uhakiki huo, madai halali ya wafanyakazi 893 yalibainika kuwa shilingi bilioni 1.024 tofauti na madai ya awali ya zaidi ya shilingi bilioni 47 yaliyokuwa yakidaiwa na wafanyakazi 1,687. Aidha, kulikuwepo na madeni ya wazabuni mbalimbali yaliyofanya jumla ya deni kufikia shilingi bilioni 1.52. Dkt. Kiruswa amesema Serikali tayari imejumuisha madeni hayo kwenye orodha ya madeni ya Serikali na kwamba Wizara ya Madini inaendelea kushirikiana na Wizara ya Fedha kuhakikisha malipo yanafanyika baada ya kukamilika kwa uhakiki wa mwisho unaoendelea kwa sasa. “Kwa sasa timu ya wataalamu inakamilisha taarifa ya mwisho ya uhakiki ili madeni hayo yaweze kulipwa na Serikali,” amesisitiza Dkt. Kiruswa.
1
3
200
Replying to @RKishaija81715
Stamico, Tanesco, TPDC & TPA
1
96
📍Bungeni, Dodoma ▪️SERIKALI KUJENGA KITUO CHA KISASA CHA UCHENJUAJI DHAHABU MWAKITOLYO ▪️Wachimbaji Wadogo Kunufaika na Kituo cha Kisasa cha Dhahabu Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) imepanga kujenga kituo cha mfano cha kuchenjua madini ya dhahabu kwa kutumia teknolojia ya kisasa katika eneo la Mwakitolyo katika mwaka wa fedha 2026/27, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuwawezesha wachimbaji wadogo kuongeza tija na thamani ya madini yao. Kauli hiyo imetolewa leo Mei 07, 2026 Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Dkt. Steven Kiruswa wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Mwanahamisi Athuman. Dkt. Kiruswa amesema ujenzi wa kituo hicho ni sehemu ya mkakati wa Serikali kupitia STAMICO wa kuwaendeleza na kuwaimarisha wachimbaji wadogo nchini. Ameeleza kuwa vituo vingine vya mfano vimejengwa katika mikoa ya Geita na Mara Mbeya. Aidha, amesema mkandarasi wa utekelezaji wa mradi wa kituo cha Mwakitolyo tayari amepatikana na kwamba hatua za mwisho za kimkakati zikikamilika, ujenzi utaanza rasmi. “Usanifu wa kituo hicho tayari umekamilika na kitakuwa na uwezo wa kuchenjua tani 120 za mbale kwa siku,” amesema Dkt. Kiruswa. Ujenzi wa kituo hicho unatarajiwa kuongeza ufanisi katika shughuli za uchimbaji mdogo, kukuza ajira pamoja na kuongeza mchango wa sekta ya madini katika uchumi wa Taifa.
3
7
324