Nimeandika na kufuta mara kadhaa.
Haya yoote yanakosa mashiko kwa kutothamini uhai wa mwanadamu. Enforced disappearances, yaliyotokea October 29 na kutokuwepo kwa nia ama utayari wa kuwajibika vinatia doa kubwa sana. Kuna mambo yanafanyika unabaki kuwaza hawa watu wanafikiria nn!
Huwezi kutaja mafanikio ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli bila kumtaja Rais Samia Suluhu Hassan, kwa sababu kwanza walikuwa wote,pili sehemu kubwa ya miradi hiyo imekamilishwa au kuendelezwa kwa kasi chini ya uongozi wake wa Rais Samia.
Ni kweli kwamba Dkt. Magufuli alijulikana zaidi kwa nidhamu kali, kasi ya utekelezaji wa miradi mikubwa, kubana matumizi ya serikali, pamoja na kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani. Hata hivyo, kulikuwa pia na changamoto na malalamiko mbalimbali, hususan katika maeneo ya demokrasia, diplomasia, na mazingira ya biashara ambapo baadhi ya wafanyabiashara walilalamikia ugumu wa kufanya shughuli zao na kufungiwa biashara zao.
Kwa upande mwingine, Rais Samia Suluhu Hassan ameonekana kujipambanua zaidi katika diplomasia, kufungua uchumi, kuimarisha mahusiano ya kimataifa, pamoja na kuendeleza miradi yote ya kimkakati iliyoanzishwa awali. Aidha, amewekeza kwa kiwango kikubwa katika sekta za huduma za afya, elimu, utalii, kilimo, ardhi, na biashara.
Kwa hiyo, inaweza kusemwa kuwa Dkt. Magufuli aliwekeza zaidi kwenye miradi mikubwa inayoonekana kwa macho na kuvutia wananchi wengi kwa haraka, jambo ambalo limekuwa kawaida kwa viongozi wengi wa Afrika wanaopenda kuonyesha maendeleo kupitia miundombinu mikubwa.
Rais Samia, kwa upande wake, ameonekana kujikita zaidi katika maboresho ya mifumo na sekta mahsusi ambazo matokeo yake si rahisi kuonekana kwa kila mtu isipokuwa kwa wadau au wanufaika wa moja kwa moja. Mfano mzuri ni maboresho yaliyofanyika katika Bandari ya Dar es Salaam na sekta ya uchukuzi,sekta ya ardhi, huduma za afya, sekta ya utalii, pamoja na upatikanaji wa mbolea za ruzuku kwa wakulima.
Mtu anayefanya kazi bandarini anaweza kuelewa mabadiliko makubwa yaliyofanyika huko. Mtaalamu wa ardhi anaweza kuona maboresho ya mifumo ya ardhi. Mgonjwa au mtoa huduma za afya anaweza kushuhudia uwekezaji mkubwa uliofanywa hospitalini na kwenye vifaa tiba. Vivyo hivyo, wadau wa utalii na wakulima wanaweza kueleza namna sekta zao zilivyoboreshwa katika kipindi hiki.
Kwa ujumla, viongozi hawa wawili wamechangia maendeleo ya Tanzania kwa mitazamo tofauti: mmoja akiwa na msisitizo mkubwa kwenye utekelezaji wa miradi mikubwa ya kitaifa, na mwingine akiwa na mwelekeo zaidi wa kuimarisha mifumo, sekta za huduma, diplomasia, na mazingira ya uchumi kwa ujumla.