Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Kenani Kihongosi, amewasisitiza wakazi wa Kata ya Puge Wilayani Nzega kuwa wazalendo namba moja wa kulinda amani ya nchi, akibainisha kuwa amani ndiyo msingi wa maendeleo ya Taifa.