π₯ππππππ ππ ππππππππππ πππππ πππ ππ πππππππππ πππππ ππ ππππ ππππ πππππππππππ ππππππ πππ ππππ πππππππππππ: πππππππππ
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Ndugu Kenani Laban Kihongosi, amesema kuwa zipo taarifa zinazodai kuwepo kwa watu wanaojaribu kuchochea migawanyiko na vurugu zinazoweza kuhatarisha amani na utulivu wa Taifa.
Ndugu Kihongosi ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kusimama imara kulinda uhuru, umoja na mshikamano wa nchi yetu, huku akisisitiza umuhimu wa kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuimarisha umoja wa kitaifa, amani na maendeleo ya Watanzania wote.
Amesema Tanzania itaendelea kuwa imara pale wananchi watakapoweka mbele maslahi ya Taifa, kudumisha upendo na kushirikiana kujenga nchi yenye mshikamano na ustawi kwa wote.
Tembelea:
ccm.or.tz
______
#KaziNaUtuTunasongaMbele
#CCMIpoKazini
#MtumishiWaWote