Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakari Zubeir Ally amemuomba Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi kumshawishi Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ili mapumziko ya Mwaka Mpya wa Kiislamu Hijiryya yawe Nchi nzima.
Mufti ameyasema hayo leo Juni 15, 2026 mbele ya Rais Dkt. Mwinyi wakati wa mwendelezo wa Maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Kiislamu visiwani Zanzibar.
โMimi nitumie nafasi hii kwamba mapumzo tunayaomba pia na kule Bara yaenee kwasababu Nchi ni moja, hii inaitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunaomba na sisi ieneee Tanzania nzima kwa kuwa Dkt. Mwinyi amethubutu kufanya jambo hili, namuomba Mungu awape zaidi Taufiq na uweze kumshauri Rais wa Jamhuri hili jambo liweze kuzagaa na kwa jambo hili ni sababu ya moja kwa moja kupata daraja la juu katika pepo,โamesema Mufti Zubeir.
Rais Dkt. Mwinyi ametangaza kuwa Jumatano Juni 17, 2026 itakuwa siku ya mapumziko kwa Zanzibar ili kuukaribisha Mwaka Mpya wa Kiislamu 1447 Hijirrya.
#MillardAyoUPDATES