Mwaka huu hatukusema tu “teknolojia kwa wakulima” tulifanya kazi ilioenda kuonekana shambani.
Mwaka 2025 tumezindua MazaoHub v2.0.2, toleo lililokuja kuoanisha Afisa Ugani na Mkulima, wauzaji wa pembejeo na wakulima, pamoja na distributors na agro-vets/agro-dealers ili huduma iwe karibu, haraka, na ya kuaminika.
Kupitia field-based data tunayokusanya kwenye mfumo wetu, wadau wengi wameweza kunufaika kuanzia taasisi za kifedha, research institutions, na taasisi mbalimbali kwenye mnyororo mzima wa thamani kwa sababu data sahihi huleta maamuzi sahihi.
Matokeo yake:
✅ Tumewahudumia wakulima zaidi ya 80,000
✅ Tumeongeza vituo hadi kufikia 17 nchini
✅ Tumeshirikiana na FECs & Agro-vets zaidi ya 420 (ikiwemo agro dealers & input dealers)
✅ Tumewapa nafasi vijana zaidi ya 200 “Uber for Extension” — wanahudumia wakulima na kujipatia kipato kupitia kamisheni na hatukuwasahau akina mama. Mwaka huu tumeweka mfumo unaowawezesha kuweka rekodi za shughuli zao za kilimo hata bila kumiliki zana za uzalishaji kama mashamba, na tumewasogezea ujuzi wa kifedha kupitia taasisi za kifedha kama CRDB Foundation ili wajue namna sahihi ya kutunza kipato hatua inayowaweka karibu zaidi na fursa za mikopo rafiki.
Kwa upande wa masoko, mfumo wetu CropSupply umeendelea kuwa daraja: umewezesha wakulima kupata masoko ya uhakika na wanunuzi 98 Afrika Mashariki kupata malighafi za uhakika.
Na sasa… 2026 tunaenda kufanya mageuzi makubwa zaidi ikiwemo uzinduzi wa CropSupply Mobile App ili masoko, ufuatiliaji, na uaminifu viwe kwenye kiganja cha mkulima.
Huu ni ushahidi kwamba kazi tumeifanya na mwaka 2026 tumejipanga kwenda kufanya mageuzi makubwa zaidi.