MPOX🫵
Dalili za Monkeypox [Mpox] zinaweza kufanana na za magonjwa mengine ya Virusi. Kwa mfano 'ndui' ya kawaida.
Dalili hizo huanza kati ya siku 5 hadi 21 baada ya kuambukizwa na tena, mara nyingi, hudumu kwa wiki 2 hadi 4. Hakuna Tiba!
Hizi hapa ni "Dalili Kuu" za Monkeypox [ Mpox ].
1. Homa kali – Joto la mwili hupanda ghafla tu.
2. Maumivu ya Kichwa nao usumbufu mkubwa.
3. Mwili Kulegea, Uchovu Mkali, Kukosa Nguvu.
4. Maumivu ya misuli, mgongo na viungo vingi.
5. Kuvimba kwa tezi [ lymph nodes ] – Uvimbaji wa sehemu za siri, makwapa na mpaka shingo.
6. Vipele na vidonda vya ngozi – Hii ndiyo Dalili maarufu zaidi. Huanza kama vipele na kugeuka kuwa vidonda vyenye kutoa usaha.
Viupele huanzia usoni, kisha kusambaa mwilini ikiwemo viganja vya mikono na nyayo za miguu na Vidonda hivyo hupitia hatua mbalimbali hadi vikauke na kuacha makovu.
Jinsi [ Mpox ] inavyoambukizwa.
1. Kugusana moja kwa moja [Direct Contact] na majimaji ya mwili, au pia vidonda vya mgonjwa.
2. Kugusana na Vitu Vichafu kama Mashuka au mavazi na hivyo haitakiwi kushiriki [ Kuvaliana ]
3. Kupitia matone ya hewa, kutoka kwa mhanga [mgonjwa] aliye na 'dalili kali' za hii Monkeypox.
4. Kupitia Wanyama Walioambukizwa na "hasa" Wanyama Pori. Na au kwa kupitia "Mizoga" yao!
Ikiwa una dalili hizi, ni muhimu tafuta huduma ya afya "haraka", kwa ajili ya uchunguzi na matibabu sahihi, na kama kuna dalili zingine sijaziorodhesha na unazifahamu, unaweza kushiriki hapa ili kutusaidia.
Ugonjwa hauna dawa ila inategemeana na, 'Kinga ya Mwili' wa mgonjwa. Punguzeni 'ngono zembe' za Uzungu wa Denda na Mabusu, usisahau Kinga ni Bora kuliko Tiba!
Mizizi✌🏾