๐Hale
1.Ufundishe moyo wako kuridhika na ulichonacho.
2.Ishi duanini kama kesho hautaiona tena.
3.Boresha mahusiano yako Na aliyekuumba wewe.
4.Tenga muda kujiuliza wewe ni nani na umetokana na nini.
5.Wapende sana wazazi wako kama wapo hai na ikiwa wameshafariki waombee.
Ukiona unapata sana, tambua kwamba kuna watu pia wanapaswa kupata kupitia wewe. Usiwe mkunjaji, wanyooshe watu na MUNGU naye atanyoosha mambo yako.
Good Morning Champ.
Huna tena hamu ya kulipiza kisasi, huna hamu ya kuthibitisha upande wako kwa watu wasiokuelewa, na huna muda wa kubishana.
Unabariki wanaondoka, unaheshimu wanaobaki, na unalinda utulivu wako kwa gharama yoyote ile.
โbasi umesha kuwa mtu mzima!
Wapo wale ndugu kila ukionana nao au ukienda kwao maswali yao huwa yanafanana na ni yale yale.
Utasikia, unaoa lini, una watoto wangapi? unataka tufe hata mtoto wako hatumjui? kwanini hupendi kutuletea Wifi /shemeji..?
Kuna muda tutaanza kuwakwepa na kutowatembelea sasa..๐ซต๐พ