Leo Tunaadhimisha historia yetu na kuenzi ukuaji wa biashara, ubunifu na maendeleo ya viwanda.Tushirikiane kujenga uchumi jumuishi. Heri ya Siku ya Saba Saba ๐น๐ฟ
#GhFoundatio#PromoteEmpowerInspire#SabaSaba#Tanzania
Tunawatakia Waislamu wote Heri ya Mwaka Mpya wa Kiislamu, 1447 Hijria. Tuutumie mwaka huu mpya kama fursa ya kujitathmini, kuimarisha imani, na kuendeleza amani, mshikamano na huruma katika jamii zetu. Hijria Njema.
#GhFoundation#PromoteInspireEmpower
Wawakilishi wa GH Foundation wanaoshiriki mkutano wa EAPN nchini Rwanda, wamepata fursa ya kutembelea ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda na kupokelewa na Balozi wetu Kigali, Mhe.Habib Kambanga.
#GhFoundation#PromoteInspireEmpower
On this Labour Day, weโre celebrating the innovation, grit, and resilience of every worker powering our world. Your hustle fuels progress and shapes tomorrow. Happy Labour Day keep forging new paths!
#GhFoundation#PromoteEmpowerInspire
Mkurugenzi wa GH Foundation, @MalisaGJ_ , amesema takwimu sahihi ni msingi wa maamuzi bora dhidi ya ukatili wa kijinsia. Ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam kwenye warsha iliyowakutanisha pamoja polisi, ustawi wa jamii na viongozi wa dini.
#GhF#PromoteEmpowerInspire
Accurate data is the backbone of smart, strategic action against gender-based violence, says GH Foundation Director @MalisaGJ_ . Speaking in Dar, he stressed data-driven policy as key addressing a workshop uniting police, social workers & faith leaders.
GH Foundation has gifted Theodory a modern bicycle at Chilombora Primary School, Ulanga Morogoro. It will serve as both a wheelchair and a classroom desk. Theodory, his mother, teachers, and classmates were all delighted!
GH Foundation imemkabidhi Theodory baiskeli ya kisasa katika Shule ya Msingi Chilombora, Ulanga โ Morogoro. Itamsaidia kama kiti mwendo na dawati darasani. Theodory, mama yake, walimu na wanafunzi wenzake walifurahi sana! #GHFoundation#PromoteEmpowerInspire#Ulanga#Morogoro
GH Foundation conveys profound Easter salutations. May this sacred season rekindle collective empathy, socio-ethical consciousness, and a renewed commitment to transformative development.
#Easter2025#GHFoundation#PromoteEmpowerInspire
GH Foundation imefanya warsha Kinondoni kuwajengea uwezo Polisi, Ustawi wa Jamii, Viongozi wa Dini & Waandishi kupambana na ukatili wa kijinsia. Lengo likiwa ni kuboresha mifumo, ushirikiano & msaada kwa waathirika. #GHfoundation#LetLoveLead#PromoteEmpowerlnspire
GH Foundation imefanya kikao na Dr. Hellen Makwani, daktari bingwa wa saratani na Mkuu wa kitengo cha saratani katika Hospitali ya Lumumba, Zanzibar, pamoja na Mkurugenzi wa Genesis Foundation. Wamekubaliana kuingia katika ushirikiano ili kupambana na magonjwa yasiyoambukiza.
Tulitembelea Shule ya Sekondari ya Salma Kikwete ambapo tulienda kutoa elimu kuhusu afya ya uzazi (SRH), kupinga ukatili wa kijinsia (GBV), na kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza (NCD). Aidha, taasisi ilitoa taulo za kike kwa wanafunzi 400.
#GHFoundation#PromoteEmpowerlnspire
The GH Foundation celebrates the achievements of women and girls worldwide. We are committed to fighting gender-based violence and non-communicable diseases to promote an equal and safe society. Happy International Women's Day!
Taasisi ya GH Foundation inasherehekea mafanikio ya wanawake na wasichana duniani kote. Tumejizatiti kupambana na ukatili wa kijinsia na magonjwa yasiyoambukiza ili kukuza jamii yenye usawa na usalama. Heri ya Siku ya Wanawake Duniani.!
Taasisi ya @ghfoundationtz juzi jumapili 5/5 ilikabidhi nyumba yenye thamani ya Milioni 52 kwa Judith Ruhumbika mjane aliyekumbana na ukatili wa kijinsia Baada ya kufiwa na mumewe kitendo kilichopelekea kufukuzwa nyumbani na watoto wake 5. Ambapo baada ya kuondoka Kahama alisafiri kuja dar na akawa hana makazi na kulazimika kuishi na watoto wake Stand ya Mabasi ya Ubungo.
Kabla ya kwenda kupanga nyumba ya Chumba kimoja Boko magengeni ambapo aliishi na watoto wake 5. Taasisi ya @ghfoundationtz baada ya kukutanishwa nae tulianza mchakato wa Kusaidia watoto wake waweze kupata Elimu Bora ambapo watoto wake tunawasomesha Mkubwa akiwa mwaka wa 3 Chuo cha Serikali za mitaa Hombolo Dodoma na wa kike yupo Pree form 5 Shule ya Sekondari ya Rosemini Tanga. Ambapo alihitimu kidato cha nne katika Shule hiyo na kupata daraja la kwanza yaani division One.
.
Pili mwaka 2021 mwishoni tulianza Ujenzi wa kumjengea nyumba ili apate makazi ya kudumu ambapo tumekamilisha na juzi jumapili 5/5 tulimkabidhi nyumba yake Rasmi. Sifa na Utukufu tunamrudishia Mungu aliyetupa maarifa ya kutenda haya๐๐
GH Foundation inakutakia Afya njema ya Figo yako. Zingatia ushauri wa Daktari mtaalamu anayetambulika. Epuka ushauri wa marafiki na watu wengine wasio na taaluma ya Afya. Epuka matumizi ya dawa zisizothibitishwa.
Tunza Figo yako.