"Katika serikali hii ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan (Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) hakuna kitakachosemwa kisisikilizwe, ndugu zangu, wazee wangu, mama zangu hapa (kijiji cha Mmawa) baada ya kupata kijiji jukumu la kwanza lilikuwa ni kuhakikisha tunaipandisha shule, tumeiorodhesha miongoni mwa shule zinazohitaji kuongezewa miundombinu lakini tulianza kwa utaratibu, utaratibu huu tulianza na shule zilizoko kando kando ya Barabara kuanzia Nanganga mpaka kule Nambilanje shule zetu zilizokuwa Barabarani ziliharibika mno zilikuwa zinatuhaibisha, tulianza kubomoa majengo yaliyochoka Nanganga tukaweka madarasa mapya, tulianza kubomoa majengo yaliyoharibika Chimbila 'A' tukaweka majengo mapya, tukabomoa majengo yaliyoharibika Nandagala tukaweka majengo mapya, tumebomoa majengo mabovu Namahema tukaweka madarasa mapya, tulibomoa jengo moja Mpumbe tumeweka jengo jipya" -Majaliwa
"Ndugu zangu wana Nkowe nimekuja na jambo zuri hapa, tunaenda kujenga madarasa sita (6) ya Nkowe shule ya msingi (shule ya msingi Nkowe imeharibika sana), tumefanya hivyo Mitope kulikuwa na majengo yameharibika kabisa wanafunzi walikuwa wanakaa kwenye maeneo mabaya kabisa sasa tumejenga vyumba vinne vya madarasa Mitope shule ya msingi, tumejenga madarasa mapya mengine pale Likunja shule ya msingi, lakini tumefanya hivyo Ruangwa mjini na nyie mmeona maghorofa shule ya msingi Ruangwa, mmeona hiyo Likangara shule ya msingi tumejenga ghorofa, tumendoa majengo yaliyokuwa yamechoka Nambiranje shule ya msingi tumeweka madarasa mapya, Kiperemende (kitongoji) hakikujenga shule mpya ya msingi, tumeenda Mbangala hakukuwa na shule sasa tumejenga shule ya msingi Mbungu na shule ya msingi Mbangala, lakini tumeenda mpaka Nangumbu, Namitegu kote huko tumejenga shule, Ruangwa kwa maendeleo inawezekana" -Majaliwa
Mbunge wa jimbo la Ruangwa ambaye pia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amezungumza hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mmawa, Ruangwa, mkoani Lindi leo, Jumatano Julai 03.2024