Mshambuliaji wa Manchester City, Erling Halaand (23) raia wa Norway rasmi amerejea mazoezini baada ya kuwa nje ya uwanja kwa majuma kadhaa kutoka na majeraha.
Kocha Pep Guardiola amethibitisha kuwa ataanza kumtumia mshambuliaji huyo kwenye mchezo ujao.
#PlusXtraUpdates
Nyota huyu raia wa Switzerland (35) aliyekuwa anakipiga katika klabu ya Sevilla kwa sasa ameamua kuachana na waajiri wake hao na kujiunga na klabu ya Al Shabab iliyopo nchini Saudi Arabia kwa muda wa mwaka mmoja mpaka Juni, 2025.
#PlusXtraUpdates
Wananchi wa Jamhuri ya Kenya ambao timu yao ya Taifa haijafuzu michuano dume ya AFCON mwaka huu, wataweza kupata darasa la namna ya kucheza michuano hiyo mubashara kupitia Tanzania na mataifa mengine makubwa yaliyofuzu LIVE kupitia television yao ya Taifa ya KBC
#PlusXtraUpdates
Nyota wa Nyasa Big Bullets ya Malawi, Yamikani Fodya ametangaza rasmi kustaafu kucheza soka la kulipwa.
Nyota huyo ambaye ni kipenzi cha mashabiki wengi wa soka nchini Malawi amestaafu akiwa na umri mdogo wa miaka 32 tu.
#PlusXtraUpdates
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Ia Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa katika kuijenga nchi hiyo kisasa wapo mbioni kuboresha usafiri wa umma kwa kuwa na mabasi ya umeme, treni pamoja na Taxi za baharini.
#PlusXtraUpdates
Viashiria vya upimaji wa utendaji kazi wa walimu kuanzia Januari hadi Desemba 2023 vimeonyesha kuna ongezeko la wanafunzi wa darasa la kwanza wanaomudu stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kutoka asilimia 35 hadi 94.4.
#PlusXtraUpdates
Mshambuliaji mpya kinda wa FC Barcelona, Vitor Roque ni rasmi sasa atavaa jezi namba 19 ndani ya klabu hiyo kuanzia hivi sasa baada ya kukamilisha rasmi dili ya kujiunga na wababe hao wa Catalunya akitokea Athletico PR ya nchini Brazil.
#PlusXtraUpdates