Ninatoa pongezi za dhati kwa mwanadiaspora Justina John kwa kufungua mgahawa wa ONJA- Taste of Tanzania-unaouza vyakula vya Tanzania katika mji wa Cardiff wiki tatu zilizopita. Nimepata fursa ya kutembelea mgahawa huo leo kabla ya mkutano na wanadiaspora. Katika mgahawa huo mbali na kutoa huduma ya vyakula, pia anatangaza utamaduni wa Tanzania kupitia muziki, picha na mapambo ya kitanzania. Vilevile anatangaza vivutio vya utalii vya Tanzania. Nimefurahi kusikia kwamba mgahawa huo umewavutia waingereza wengi ambao wamewahi kutembelea nchi za Afrika Mashariki pamoja na wanadiaspora kutoka nchi za Afrika Mashariki. Ninamtakia kila la kheri na kutumainia kwamba biashara yake itapanuka hadi katika miji mingine ya Uingereza.