Mdau wa
JamiiCheck.com alihitaji kujua Uhalisia wa picha inayodaiwa kuwa ya Mkuu wa Kituo cha Polisi Kabwe, wilayani Nkasi, anayedaiwa kushambuliwa na wananchi.
JamiiCheck imefuatilia picha hiyo kwa kutumia
#GoogleImageSearch na kubaini kuwa picha hiyo si ya Tanzania, kwani gari inayoonekana kwenye picha mbele ya mwanaume aliyepigwa lina nembo ya Polisi wa Afrika Kusini.
Aidha, kwa mujibu wa TimesLive, mnamo Oktoba 18, 2021, mwanaume huyo kwenye picha alijitambulisha kama Shiba na kudai yeye na wenzake wawili walishambuliwa na Polisi wa kituo cha Tshwane, Oktoba 2, 2021, walipokwenda kuchukua gari lao lililokamatwa.
Tukio la kushambuliwa kwa Mkuu wa Kituo cha Kabwe lilitokea Septemba 11, 2023, ambapo taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, ACP Shedrack Masija haikumtaja jina wala kuweka wazi picha ya afisa huyo
Soma
jamii.app/MkuuWaKituoKushamb…
#JamiiCheck #HakikiTaarifa #FactsCheck #FactsChecking #VisitJamiiCheck