#TajiriLaKihaya
Sisi Waislamu na WAKRISTO inabidi Tuunganeโฆ. Uislamu haujawahi kuwa na uadui na Ukristo hata siku moja!
Inabidi tuungane kuwatokomeza hawa wazayuniโฆ
Ukisoma Qurโan na biblia mitume wote walikuwa wanapinga Kuabudu SANAMUโฆ
Ni Propaganda tu za Wazayuni ndio zinajenga chukiโฆ
Miongoni mwa watu Wayahudi (sio wazayuni) na Wakristo ndiyo waliyo karibu zaidi na Waislamu na wao wamepewa cheo cha kuitwa watu wa Kitabu- AHLUL KITAB.
Ahlul kitaab tuna imani ya Mungu Mmoja Allah-Mtukufu na waliopokea maandiko kutoka Kwake, Taurati kwa Nabii Musa na Injili kwa Yesu (Nabii Isa bin Mariamu).
Wote tuna imani katika mlolongo wa unabii, na wengi katika marafiki zetu Mayahudi na Wakristo hushangazwa wanaposikia kuwa manabii wanaotajwa katika Biblia pia ni manabii katika Uislamu.
Dini hizi tatu zina kanuni za kimaadili zinazofanana.
Qurโan inasema; (Al-Baqarah: 136)
"Semeni nyinyi: Tumemwamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyoteremshiwa sisi, na yaliyoteremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zake, na waliyopewa Musa na Isa, na pia waliyopewa Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi; hatutafautishi baina ya yeyote katika hao, na sisi tumesilimu kwake."
Waislamu wanaruhusiwa na Uislamu kula chakula cha watu wa Kitabu (isipokuwa kile kilichoharamishwa kama vile pombe au nyama ya nguruwe) na Waislamu wanaweza kufanya vivyo hivyo kwa kuwapa chakula chao,
Mwislamu mwanamume anaruhusiwa kumchukua Mkristo anayefuata mafundisho sahihi ya Nabii Isa bin Mariamu kama mke kwa kumwoa (uhusiano uliyo wa karibu mno uliyo barikiwa)n na Katika hali hiyo itakuwa haramu kwa mume Mwislamu kumlazimisha mkewe kuingia katika Uislamu, kwani itakuwa ni kinyume na agizo la Qurโan; (Al-Baqarah: 256).
" Hapana kulazimisha katika Dini."
Kwa hakika utakuwa ni wajibu wake wa kidini kuhakikisha haki za mkewe kuabudu kwa mujibu wa imani yake.
Waislamu wameonywa dhidi ya vitendo vya ubaguzi au kisasi au chuki kwa Watu wa kitabu, na Mtume Muhammad (S.A.W) amesema:
"Yeyote atayemdhuru mtu miongoni mwa Watu wa kitabu ni kama vile kanidhuru mimi mwenyewe."
Kwa mtazamo wa Uislamu watu wote ni sawa mbele ya Mwenyezi Mungu na hakuna mtu au kundi kinachoweza kudai kuhodhi rehema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu au kuwanyima wengine,
Qurani inasema: (Al-Baqarah: 62)
" Hakika Walio amini, na Mayahudi na Wakristo, na Wasabai; yeyote atakaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na akatenda mema basi watapata malipo yao kwa Mola wao Mlezi, wala haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika. ."
Wakristo na Waislamu tuna mengi yanayotuunganisha kuzidi yanayo tutenga!
TUUNGANE๐ค