Matukio Baada ya Uchaguzi 2025: Namna Majirani Nane Walivyouwawa Kinyerezi Dar es Salaam
Mpaka sasa kunguru na nzi wamezuka eneo ambapo majirani nane wa mtaa wa Kanga-Kariakoo, Kinyerezi, jijini hapa, walipouwawa. Kabla ya mvua kunyesha Novemba 4, 2025, harufu ya kifo ilikua ndiyo alama ya eneo hilo. Mvua iliweza kusafisha baadhi ya mabaki ya viungo vya binadamu yaliyokuwa yamebaki, ikiwemo damu nzito.
Tukio hili lilitokea usiku wa kuamkia Novemba 3, 2025, majira ya saa tisa. Majirani hao waliuwawa zamu kwa zamu kwa kupigwa risasi. Hii ni baada ya kuambiwa wajilaze nyuso zao zikiangalia ardhi, na kuamrishwa kusali sala ya mwisho.
Majirani hao ambao nyumba zao zimefuatana katika mstari mmoja, walikuwa ni afisa polisi mstaafu, walimu wawili, dereva, wauza duka wawili, afisa wa benki na mfanyabiashara ndogondogo.
“Hapa kulikua hakufai kabla ya hii mvua kunyesha, wao walikuja wakamwagia mchanga, lakini kulikua hakufai, mvua imesafisha safisha, kidogo,” moja ya majirani alitueleza hali baada ya mauaji hayo.
Tukio hili lilianza baada ya duka la jumla lililopo katika mtaa huo kusikika kuwa limevamiwa na vibaka. Polisi mstaafu aliwaongoza majirani wenzake kwenda kuimarisha ulinzi katika eneo hilo, ambapo pia aliamua kupiga simu na kuita polisi.
Polisi wenye silaha walivyofika kwenye eneo hilo waliwaamrisha wote kulala chini. Licha ya kujitetea, hoja zao hazikuweza kufua dafu. Waligawanywa makundi mawili, wakitenganishwa na barabara ambayo imegawanya makazi yao, upande wa kulia na kushoto, wengine wakawekwa karibu na duka hilo la jumla, na wengine wakawekwa upande wa pili, pembeni ya nguzo ya umeme.
Soma Zaidi>>>
thechanzo.com/2025/11/09/mat…